Friday, September 14, 2012

SIKU YA IJUMAA HALI HALISI

Railoni likiwa limetandikwa kabla ya zege kumwaga.Railoni hii husaidia katika swala la Nondo kutokugusana na mawe.Mawe huozesha nondo kwa maji maji yake na ukungu unakuwa umebaki.

                          Sehemu  ilimwagwa zege inavyoonekana kwa sasa

Baadhi ya Wana Moyo Mtakatifu wa Yesu waliofika kuangalia shughuli za Ujenzi. Kutoka kulia ni Mzee Nkondola,Bibi Mbotto,Mzee Mongela,Fratel na Mama Khadija

Baba Paroko akifafanua jambo kuhusu Ujenzi kwa Mzee kasela alipokuwa katembelea shughuli za kanisani.

Fundi umeme akijadiliana mambo kadhaa na Baba Paroko na Mzee Kasela

Katekista akiangalia T shirt ambazo tunapaswa kuvaa siku ya Uwekwaji wa Jiwe la Msingi tarehe  22/09/.
T shirt moja ya Mkubwa ni 20000/=
Ya watoto ni                        10000/=
na Vitenge ni                       15000/=
Hima Baba,Mama na Vijana siku hiyo tuwe kwenye sare moja. T shirt zipo parokiani kwa bei hiyo na hata kupitia viongozi wetu wa kanda na jumuiya. Pia waweza weka order kupitia kwa viongozi wako.Kumbuka kununua T shirt hizi unakuwa umeshiriki vyema kwenye kuweka jiwe la Msingi


Baadhi ya Viwawa waliofika kwenye Misa ya Asubuhi mara baada ya misa.Kutoka kushoto ni secilia,Fratel,Frida,na Claudia

                              Kutoka kulia secilia,Fratel,Frida na Paulo









No comments:

Post a Comment