Sunday, December 16, 2012

SIKU YA KUMPA MKONO BABA TALEMWA

Leo ilikuwa ni siku ambayo kila mtu parokiani alishikwa na majonzi kwa kumpa mkono Padri Gaudence Talemwa baada ya kuhitaji kuludi katika kituo chake cha  kazi.Alikuwa nasi kwa muda mrefu alipokuwa akifanya Masomo yake Chuo kikuu na baada ya kuhitimu amehitajika kuludi kwa Baba Askofu jimboni mwake
Zifuatazo ni picha alipokuwa na watoto katika kuwapa mkono wa neema na kuwaombea Baraka kwa Mungu hasa katika Masomo yao na katika Malezi wapokuwa na Wazazi
                            Watoto wakimpa mkono waKheri Baba

                           Familia ya dada paulo nayo haikuwa nyuma



 Baba akitoa neno la Shukrani na kuwaahidi kwamba ataendelea kuwatembelea na kuwaombea kwa Mungu ili wawe watoto wazuri

 Familia ya Picket Millandal  wakiwa katika picha ya pamoja na Baba Talemwa

         

               LEO ILIKUWA NI SIKU YA SEMINA KWA VIJANA PAROKIANI

Semina ya leo ilitolewa na Katekista wetu Ndugu Shayo katika ukumbi wa Parokia,ingawa mada zilikuwa chache lakini zilikuwa nzuri na zakuelezeka na kuelewa
Zifuatazo ni mada Tulizojadili katika Semina
  •                IMANI
  •                UHUSIANO NA MUNGU
  •                EKARISTI
  •                MAUNGAMO
Katika yote tulikumbushwa na Katekista kuwa huu ni mwaka wa Imani na hasa unatulenga sisi Vijana kwani ndo Taifa ambalo linategemewa kwa miaka ijayo katika kuendeleza Taifa la Mungu

Zifuatazo ni picha wakati wa semina



 Emmanuel Lufunga(katibu mwenye tshirt ya njano)akifungua Semina na huku Mjumbe wa kamati ya Litrujia akiendelea kuandaa masomo
                          Katekista akiendele kutoa semina kwa Vijana
  Baadhi ya Washiriki walioshiriki kwenye Semina wakifatilia Semina kwa umakini zaidi  na kunukuu baadhi ya vitu
 Vijana wakifurahi kwa Mada zilivyopamba moto kuhusu mahusiano na Mungu
Hawa ni baadhi ya vijana walioshiriki kwenye semina mpaka mwisho katika picha ya pamoja na Mlezi wetu Baba G Talemwa
              

No comments:

Post a Comment