MAANA YA VIWAWA NA HISTORIA YA VIWAWA .
MAANA YA VIWAWA.
Viwawa
maana ya Viwawa ni Vijana Wakristo Wakatoliki(Wengine wanasema ni
Vijana Wakatoliki Wafanyakazi) Viwawa ni chama cha kitume cha Vijana
ndani ya Kanisa ambao wanatumwa na Yesu mwenyewe kuendelea kazi yake
kwa watuwake kwamba yeye “NDIYE NJIA YA KWELI NA UZIMA”Kwa Vijana wote
katika maisha yao ya kila siku.
HISTORIA YA VIWAWA KIDUNIA.
Viwawa
ilianzishwa mwaka 1924 mji wa Brussel nchini Ubelgijina Padri Joseph
Cardjin na kupitishwarasimi na kama chama cha kitume cha vijana
Kimataifa na Balaza la Kipapa Vatican mwaka 1950.Padri Joseph Cardjin
pia alianzisha YCS,hivyo VIWAWA Na YCS alianzisha yeye.Makao makuu ya
VIWAWA Duniani yako Roma-Italia chini ya Rais Seraphina kutoka
Korea,Katibu Mkuu Jules Adached toka Bejin,Mhazini Lisa Vaccariano toka
Italia na Mratibu wa kimataifa Arniel Iway toka Philipini na mshauri
Pd.Joseph Ramaguera toka Spain.
HISTORIA YA VIWAWA TANZANIA.
Viwawa
Tanzania iliingia mwaka 1959 katika Parokia ya Msimbazi,Jimbo kuu la
Dar es salaam chini ya Mwanzilishi Padri Hendrikus Johannes Brinkhof
maarufu kama Padri Mansuetus na kupitisha rasimi chama cha Kitume cha
Vijana na Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) mwaka 1979.Baada ya kupitisha
hapo kilitambulishwa pote Tanzania kama chama cha Vijana Wakatoriki
Wafanyakazi Tanzania(VIWAWA).
Mpaka sasa chama hiki kipo kipo majimboni,kuanzia ngazi ya Jumuiya,Mtaa,Kanda,Kigango,Parokia,Kijimbo,Taifa na Kimataifa.
LENGO LA CHAMA.
-Kumuezesha Kijana awe mkristo wa kweli na raia wengine waweze kurekebisha,Kuendeleza na Kudumisha taratibu za uchumi,utamaduni,ustawi,siasa na utaalamu kufatana na mpango wa Mungukatika kutafakali injili na kusali.
-Kuunda umoja na ushirikiano kwa vijana kadili ya injili na mafundisho ya Yesu Kristo.
-Kuishi
upendo wa Kikristo kama watoto wa Baba mmoja.Hii ni amri ya Yesu “Amri
mpya nawapa pendaneni kama vilenilivyowapenda ninyi,nanyi mpendane vivyo
hivyo.(Yoh 13:34-35).