Sunday, February 17, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KANISA

Balozi wa Baba Mtakatifu Nchini Tanzania anayofuraha kutangaza kwamba Baba Mtakatifu Benedicto XVI amemteua Mheshimiwa Padri Titus Joseph MDOE wa Jimbo la Tanga kuwa Askofu wa Jimbo la Heshima la Baanna na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam.
Askofu Mteule Titus Joseph MDOE alizaliwa Ngulu tarehe 19 Machi 1961 katika Parokia ya Gare Wilayani Lushoto. Alipata elimu ya msingi huko Kongei (1968-1974) na elimu ya Sekondari katika Seminari ya Mtak.Petro, Morogoro (1975-1978). Elimu ya Falsafa katika Seminari Kuu ya Kibosho (1979-1981) na teolojia katika Seminari Kuu ya Mtak. Karoli Lwanga Segerea (1981-1986). Askofu Mteule alipata Daraja ya Upadre tarehe 24 Juni 1986.
Baada ya kupata Daraja ya Upadri, Askofu Mteule ametoa huduma sehemu mbalimbali: Paroko Msaidizi Parokia ya Gare (1986-1987), Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kilole (1987-1989), Mkurugenzi wa Miito na Vijana (1988), Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kanisa Kuu (1989-1992), Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mt.Teresia, Tanga na Mkurugenzi wa Miito na Vijana (1992-1994), Paroko wa Parokia ya Hale (1995-2000), Masomo ya Juu nchini Marekani (2008-2009), Mwalimu Seminari ya Soni pia Mkurugenzi wa Miito na Vijana (2009-2010). Hadi alipoteuliwa, Askofu Mteule alikuwa ni Naibu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha wa Chuo cha Mt.Augustino (SAUT) Kituo cha Mtwara.

No comments:

Post a Comment