Hakika leo ni siku ya kumshukuru muumba,kwani kwa mara ya kwanza Parokia ya makongo juu ilipokea wageni kutoka parokia ya Kigogo
Karibu tuangalie matukio katika picha
Hapa ni MC Eusebius Francis akiwakaribisha wageni kwenye ukumbi wa Parokia akiwa na kaka Samsoni felix
Walezi wetu Ndugu Robert Millandal na Mama Jane Mfungahema
Walezi kutoka Parokia ya Kigogo
Baadhi ya Vijana walioshiriki kutoka Parokia ya kigogo
Baadhi ya Utoto Mtakatifu walioshiriki kwenye Kongamano la Mahenge mwaka huu
Kijana kutoka Parokia ya Kigogo akichangia mada
Dada Sala kutoka Parokia ya Makongo juu akichangia mada
Baba Paroko Padri Mvungi akijaribu kuweka sawa jambo kuhusu mada
Mwenyekiti wa Vijana Makongo juu akichangia mada
Kamati ya kutunisha Mfuko wa Ujenzi hawakuwambali.Mlezi akichangia mfuko chakavu katika sherehe yetu
Mama mlezi naye akisoma swali na kujiandaa kuchangia Mfuko wa Ujenzi wa Vijana
Eva na Crispin wakiwa wameenda kumsaidia Mama yao kujibu swali la Biblia
Hawa nao hawakuwa mbali katika kuchangia ujenzi wa kanisa
Kawa kawaida Michezo iliendelea na hapa wadada wakichuana kunywa Soda,kutoka kushoto ni Sala ambaye aliibuka kidedea akiwakilisha Parokia ya makongo juu
Hapa napo wakaka wakichuana,lakini walijikuta wakimaliza pamoja na hivyo kuwa droo
Michezo iliendelea,lakini kwa hapa hakuna aliyebahatika kushika katika kuotea
Vijana kutoka Parokia ya kigogo wakituburudisha kwa Igizo
Igizo likiwa limekolea
Hamadi fumanizi katika Igizo
Wana Makongo nao hawakuwa mbali kwa Maigizo
Mke na Mume wakitafakari jambo kuhusu maisha yao ya Ndoa
Kamati ya Msosi ikiwa imejipanga vyema kutuudumia
Walezi wetu wakienda katika kujitetea kwa haki ya kila Mwanadamu
Utoto Mtakatifu wakiwa kwenye foleni ya chakula
Utoto Mtakatifu wakitumbuiza mbele ya wageni Rasmi na Vijana kwa ujumla
Hapa tukiwa uwanjani kujiandaa kwa michuano,na hawa ni baadhi ya vijana wa Parokia ya kigogo
Walezi wakifatilia Mpira wa Miguu kwa makini
Vijana nao katika shwangwe ya kushangilia
Timu zikiendelea kumenyana ambapo Parokia ya Makongo juu waliibuka kidedea kwa magoli 2 na kigogo 0
Mwenyekiti Adam Kapilima akifalia Mpira kwa makini zaidi
SHUKRANI ZA DHATI
Wale wote waliojitolea kwa Hali na Mali
Vijana wote walioshiriki
wazazi pia waliowaruhusu watoto wao
na zaidi kwa walezi wote
Hatuna cha kuwalipa ila Mungu awabariki sana